Mwelekeo wa Halmashauri ya Manispaa, ni kuendeleakuboresha na kutoa huduma endelevu za kijamii na uchumi, kuimarisha amani na utulivu, kulinda na kuhifadhi mazingira, kuwezesha jamii kusimamia maendeleo yao wenyewe na kupiga vita umaskini.
Dira ya Manispaa ya Dodoma katika kipindi cha miaka kumiijayo, inadhamiria kuboresha huduma za kiuchumi, na kijamii,kuimarisha utawala bora, kulinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu. Haya yote yanawahakikishia wawekezaji hali ya ulinzi na usalama.