HISTORIA YA DODOMA
Miaka mingi iliyopita mji huu ambao unaitwa Dodoma ulikuwa ukifahamika kama Calangu (Chalangu) mji huu haukuwa na wenyeji bali ulikuwa na wahamiaji toka maeneo mengine ambao ni wamanghala, wabambali, wayenzele na wanghulimba. Wahamiaji hawa walikuwa wakitofautiana kwa tabia zao, wamanghala na wabambali waliishi msituni na walikuwa wawindaji wakila nyama na asali. Na wayenzele na wa wanghulimba walikuwa wakulima na wafugaji. Watu hawa walikuwa waoga kiasili hivyo watu wengine walipoanza kuingia kutoka maeneo ya kaskazini wambugwe, magharibi wanyamwezi na kusini wa hehe watu hawa waliondoka na kwenda kuishi sehemu nyingine. Sababu ya wahamiaji hawa kuitwa wagogo, inatokana na wafanyabiashara wakinyamwezi walipokuwa wakipita na bidhaaa zao kuelekea Pwani kwa biashara, walipofika kati ya Itigi na Manyoni walikuta mti mkubwa umeanguka na kuzuia njia, hivyo kwa muda mrefu wali lazimika kulala upande mmoja kabla ya kuvukia upande wa pili wa mti (gogo). Hii iliwafanya kila walipoulizwa wanalala wapi kabla ya kuendelea na safari walisema wanalala kwenye limgogo. Kwa hiyo wahamiaji hawa wakafahamika kama gogo (wagogo) kutokana na gogo hilo. Mnamo mwaka 1912 alifika mjerumani Dr. Spreling (Spelenje), na kuanzisha ngome yake, ngome hiyo kwa sasa ni ofisi ya Waziri Mkuu. Ofisi aliyokuwa akifanyia kazi za utawala na utoaji maamuzi kwa wahalifu (kufungwa, kuchapwa viboko na kunyongwa) kwa sasa ni Ofisi ya CCM Wilaya ya Dodoma Mjini. Bustani aliyopenda kutembelea na kupumzika ilikuwa eneo la Kikuyu ambayo kwa sasa ni Chuo Kikuu cha St. John’s, eneo hili kwa wakati huo lilikuwa tepetepe na mapitio ya wanyama watokao mbuga za kaskazini (Arusha) kuelekea mbuga za kusini (Mikumi). Mapitio ya wanyama hao ndio yaliyosababisha kubadilika kwa jina la eneo hili baada ya tembo kudidimia katika eneo hilo tepetepe karibu na shule ya sekondari mazengo ambayo sasa ni chuo kikuu cha St. Johns. Tendo hili la kudidimia kwa lugha ya Kigogo linajulikana kama IDODOMIA hivyo baada ya kitendo hiki jina likabadilika kutoka Calangu (Chalangu) nakuwa Idodomia (DODOMA).
Mji wa Dodoma ulitangazwa rasmi kuwa makao makuu ya Chama na Serikali chini ya kifungu cha sheria No.320 ya mwaka 1973. Baada ya hapo matukio ya mafanikio yalifuata. Mwaka 1980 mji wa Dodoma ulipewa hadhi ya kuwa Manispaa. Mwaka 1995 serikali iliamua kuwa shughuli zote za bunge zifanyikie Dodoma. Bunge lilianza shughuli zake rasmi mwezi Februari 1996.
ONGEZEKO LA WATU
Halmashauri ya Manispaa ina jumla ya wakazi (watu) 462,968 wakiwemo wamaume 227,978 na wanawake 234,990 wastani wa ongezeko la watu kwa 4.0% ukilinganisha na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 ambayo jumla ya watu ilikuwa 324,347 wakiwemo wanaume 157,469 (48.5%) na wanawake 166,878 (51.5%).
MAHALI ILIPO
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ina ukubwa wa kilometa za mraba 2769 ipo latitudo 6.00˚ na 6.30˚ kusini longitudo 35.30˚na 36.02˚ mashariki. Mwinuko kati ya mita 600-1000 juu ya usawa wa bahari. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 196,000, eneo la malisho ni hekta 44,028 na eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 3,000. Halmashuri ya Manispaa inezungukwa na wilaya ya Chamwino kwa upande wa mashariki na wilaya ya Bahi kwa upande wa magharibi.
HALI YA HEWA
Hali ya hewa ya Dodoma ni ya kati/wastani (nusu jangwa) imegawanyika kwa majira mawili (2), ma jira ya mvua (masika) na majira ya ukame wa muda mrefu (kiangazi). Majira ya mvua huanza mwishoni mwa mwezi novemba mpaka mwishoni mwa mwezi aprili. Wastani wa mvua kwa mwaka ni kutoka 550-600mm na wastani wa joto ni kati ya 10˚C mwezi julai hadi 20˚C mwezi Novemba. Mwezi julai ni baridi sana wakati mwezi ni joto kali lisilopungua 30˚C kwa siku.
ARDHI NA MATUMIZI YAKE
Halmashauri ya manispaa ardhi yake ina rutuba ya wastani yenye udongo unaopitisha maji kiasi eneo linalo tumiwa kwa kilimo ni hekta 145,240. Yakiwemo mazao ya biashara kama zabibu hekta 2257 , ufuta hekta 9924, alizeti hekta 19,992 na karanga hekta 18,463 ambazo huleta jumla ya hekta 50,636. Hekta 94,604 zilizobaki ni kwa mazao ya chakula yaani mtama, uwele, muhogo, mahindi, viazi vitamu, kunde, njugu mawe.
26.
Mtumba

RAMANI YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA DODOMA. |
Wilaya ya Dodoma Mjini imegawanyika kiutawala katika kata 37:
1.
Chang’ombe
2.
Chamwino
3.
Chihanga
4.
Dodoma Makulu
5.
Hazina
6.
Hombolo
7.
Ipala
8.
Ipagala
9.
Kikombo
10.
Kikuyu Kusini
11.
Kikuyu Kaskazini
12.
Kilimani
13.
Kiwanja cha Ndege
14.
Kizota
15.
Madukani
16.
Majengo
17.
Makole
18.
Makutupora
19.
Mbabala
20.
Mbalawala
21.
Mnadani
22.
Miyuji
23.
Mkonze
24.
Mpunguzi
25.
Msalato
27.
Nala
28.
Ng'ong'ona
29.
Ntyuka
30.
Nzuguni
31.
Tambukareli
32.
Uhuru
33.
Viwandani
34.
Zuzu